Serikali iko katika hatua za mwisho za kukamilisha Mfumo wa Kidijitali wa Utoaji wa Taarifa na Maoni kuhusu maafa yanayoweza kutokea, pamoja na namna ya kuyakabili kwa haraka na ufanisi.
Mfumo huo unalenga kuimarisha uratibu, ukusanyaji na usambazaji wa taarifa muhimu zitakazosaidia kuzuia au kupunguza madhara yatokanayo na maafa.
Mfumo huo utakuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maafa, na unatarajiwa kuwa jukwaa kuu la mawasiliano kati ya serikali, wadau wa maafa na wananchi kwa ujumla.
#AzamTVUpdates
✍Joseph Mpangala
Mhariri | @claud_jm