Viongozi wa Iraq wamesisitiza mchango muhimu wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani katika kuliangamiza kundi la kigaidi la Daesh kulinda mafanikio ya ushindi huo.

Msisitizo huo umetolewa katika kumbukumbu ya miaka sita ya kuuawa shahidi kwa makamanda wa ushindi iliyofanyika Baghdad, mji mkuu wa Iraq, ambapo sambamba na maafisa wa ngazi za juu wan chi hiyo kusisitiza uungaji mkono wa Iran, kuhifadhi mafanikio ya vita dhidi ya ISIS, na kuimarisha umoja wa kitaifa, waliwaenzi makamnada wa muqawama mashahidi Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis.

Hauli hiyo iliyofanyika Jumapili ya jana ilihudhuriwa na Marais, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge la Iraq na shakhsia wengine wa kidini na kisiasa wa nchi hiyo.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani Abu Mahdi al Muhandis, waliuawa shahidi Januari 3, 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad

Akihutubia katika hafla hiyo, Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia al-Sudani, , alisifu jihadi na mapambano ya mashahidi, Luteni Jenerali Hajj Qassem Soleimani, aliyekuuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Vikosi vya vya Wananchi wa Iraq cha al-Hash’d al-Sha’abi, akisema kwamba,  maisha ya shahidi Soleimani yalimalizika kwa kuuawa shahidi katika ardhi ya Iraq na kwamba makamanda hawa walikuwa na nafasi muhimu katika operesheni ya ushindi dhidi ya kundi la kigaidi la ISIS.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliuawa shahidi Januari 3, 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, aliyekuwa Naibu Mkuu wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya al Hashd al Sha’abi na wanamapambano wengine wanane, wakati alipoelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *