
Vyombo vya habari vya Israel vimekiri kwamba, lengo la Rai wa Marekani Donald Trump la kuanzisha shambulio la kijeshi dhidi ya Venezuela halikuwa kupambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya bali kupora rasilimali za nchi hiyo.
Vyombo vya habari vya Kiebrania vimekiri waziwazi kwamba dawa za kulevya kilikuwa kisingizio tu cha Trump kuweka mhimili wa mafuta chini ya mzingiro.
Vyombo hivyo vya habari viliongeza kuwa, vita halisi vilivyo nyuma ya pazia ni vita dhidi ya rasilimali za nishati za Venezuela.
Vyombo vya habari vya Kizayuni vilisisitiza kwamba kilichotokea Venezuela Jumamosi asubuhi kilikuwa mgogoro mkubwa kuhusu rasilimali za nishati na teknolojia za hali ya juu.
Zaidi ya watu 40 waliuawa katika mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya Venezuela siku ya Jumamosi, wakiwemo raia na wanajeshi, gazeti la New York Times limeripoti, likimnukuu afisa mkuu wa Venezuela ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Baada ya vikosi vya Marekani kushambulia Caracas mapema Jumamosi, na kutekwa nyara kwa Maduro, Mahakama ya Juu ya Venezuela ilimteua Makamu wa Rais, Delcy Rodríguez kama rais wa muda ili kuhakikisha kuwa hakuna ombwe la uongozi na kuunda Baraza la Ulinzi la Taifa la nchi hiyo.
Mataifa mbalimbali duniani yameendelea kulaani vikali mashambulizi hayo ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Venezuela. Nchi hizo zimeeleza wasiwasi wao kuhusu uhalali, maadili na taathira hatari za uvamizi wa Marekani huko Venezuela.