Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama amekosoa vikali uzembe wa Ulimwengu wa Kiislamu kuhusiana na hali ya Ukanda wa Gaza.

Akizungumzia hali mbaya ya wakazi wa Gaza kutokana na vitendo vya kikatili vya utawala wa Kizayuni na kuzorota kwa hali yao wakati wa msimu wa baridi, Sheikh Maher Hammoud Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Muqawama amekosoa vikali kutochukua hatua kwa ulimwengu wa Kiislamu na kusema: “Hali na mazingira mabaya huko Gaza yanatokana na kushuka kwa thamani za kidini.”

Sheikh Maher amebainisha kuwa, hali mbaya ya wakazi wa ukanda huo haitokani na baridi kali, mvua, na uharibifu wa nyumba zao tu, bali ni kutokana na kupungua kwa thamanai za kidini hali ambayo imeenea katika ulimwengu wa Kiislamu na kuufikisha umma wa Kiislamu katika hali hii ya ukosefu wa dhamira za kiutu.

Wapalestina wa Gaza wakiwa katika mgawo wa chakula cha msaada

Akizungumzia ukosefu wa vifaa vya msingi vya kuishi huko Gaza, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa umeme na vifaa vya kutia joto wakati wa msimu wa baridi na mvua kubwa, Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulamaa wa Muqawama aliongeza: “Wapalestina huko Gaza wanaishi katika mazingira magumu chini ya mahema. Maji ya mvua yameingia kwenye mahema yao, huku wakinyimwa huduma za afya na vifaa vya awali na vya kimsingi vya kuishi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *