Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega ameagiza waalimu wakuu wa shule zote za msingi na sekondari wilayani humo kuanza kutumia mfumo wa kidijitali wa taarifa za shule ulioboreshwa, maarufu kama SIS, pindi muhula mpya wa masomo utakapoanza Januari 13 mwaka huu.

Amesisitiza kuwa ifikapo Januari 15, shule zote za serikali na binafsi zinapaswa kuwa zimekamilisha ujazaji wa taarifa zote muhimu kwenye mfumo huo, hatua inayolenga kuboresha ukusanyaji wa takwimu, ufuatiliaji wa maendeleo ya elimu na kuongeza uwajibikaji katika usimamizi wa shule.

#AzamTVUpdates

✍Juma Kapipi
Mhariri | @claud_jm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *