Kocha wa Simba Steve Barker amedai kutoridhidhwa na kiwango walichoonyesha dhidi ya Fufuni licha ya kuwa waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Barker amesema hawakupata muda mwingi wa kufanya mazoezi pamoja huki wachezaji wengi walioanza walikuwa wachezaji vijana ambao wamempa nafasi ya kuona uwezo wao na mchango wao kwa timu.
Kocha huyo ameahidi kujiandaa vyema na kufanya vizuri dhidi ya wapinzani wake atakaokutana nao kwenye nusu fainali Azam FC ambao walikwisha poteza dhidi yao kwenye Ligi Kuu Bara.