#HABARI: Kampuni ya michezo ya kubashiri Bangbet kwa ushirikiano na Mixx by Yas leo Desemba 8, wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa promosheni kubwa ya “Nogesha na Bangbet”, iliyobuniwa kuleta msisimko na burudani kwa mashabiki wa soka kipindi hiki cha michuano ya AFCON.
Katika hafla hiyo, washindi 10 wa juu walijinyakulia zawadi ikiwemo televisheni za inchi 55 na pesa taslimu, huku zaidi ya washindi 200 wakipokea zawadi mbalimbali kupitia promosheni hiyo iliyoweka rekodi kwa ushiriki mkubwa.
Mshindi mkuu Bw. Ndebile Paulo kutoka Singida alijishindia TSh milioni 5 na runinga kubwa ya kisasa, akifuatiwa na washindi wengine kutoka Dar es Salaam Bw. Manoni William na Bw. Bakari Said waliokabidhiwa televisheni.
Zawadi hizo zilitolewa kwa ushirikiano wa Mixx by Yas, kupitia kwa Meneja Biashara Bw. Fabian Falician, pamoja na Meneja Masoko wa Bangbet Bw. Lusekelo Mwandenene. Hafla hiyo ilipambwa pia na uwepo wa Balozi wa Bangbet, Miss Grand Tanzania Bi. Beatrice Alex, aliyeungana na washindi kusherehekea ushindi wao.