Msanii wa Bongo Fleva @iamlodymusic amezungumzia tetesi zinazodai kuwa hana ushirikiano na wasanii wakubwa kwa sababu ya tabia ya “kuvimba”. Amedai uvumi huo si wa kweli na kwamba watu wanaosema hivyo hawamjui vizuri bali ni wazushi wanaomchafua, hali inayomharibia jina na kuathiri maendeleo ya muziki wake.
Ameongeza kuwa msanii @whozu_ ni mmoja wa watu ambao huwa anawasiliana nao mara kwa mara, akithibitisha kuwa ana mahusiano mazuri na baadhi ya wasanii wakubwa.
Kuhusu collabo, Lody amesema anaamini kuwa mwaka 2026 ndio umeanza na wakati ukifika kila kitu kitaenda sawa.
Cc @missloloh_ @djfantastic255
#TheSparkShow
#Clouds26Nyoosha