@iamlodymusic akieleza sababu zilizofanya aachane na uongozi wake alioupata baada ya kibao chake “Kubali” kufanya vizuri.

Kupitia TheSpark ya Clouds TV, Lody ameeleza kuwa baada ya kupata uongozi mpya, kulizuka sintofahamu na kutoelewana ambapo alihisi hawakuwa wakimsikiliza au kumuelewa kile alichokuwa anakihitaji kwa wakati. Kutokana na hali hiyo, walishindwana na hatimaye akaamua kurejea kwa uongozi wake wa awali ambao ndiye anaendelea nao hadi sasa.

Lody amesema kuwa kwa sasa mipango yao imekaa vizuri na mashabiki wake wategemee mambo mazuri mwaka 2026.

Cc @missloloh_ @djfantastic255

#TheSparkShow
#clouds26nyoosha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *