Wananchi wa Jiji la Dar es salaam wamehimizwa kujitokeza kwa wigi kufanyiwa vipimo na kufanyiwa matibabu bure katika Kampeni ya Upasuaji wa Mabusha inayofanyika katika Mkoa huo kuanzia Januari 5 hadi 30 ,2026
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ,Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Saadi Mtambule amesema kampeni hiyo itawafikia wanachi zaidi ya 500 huku akiwakaribisha wanachi wa mikoa ya Jirani na Dar es salaam kama Lindi ,Mtwara ,Morogoro,Tanga Kujitokeza kwa wingi Kuchangamkia fursa ya Matibabu hayo.