Wamiliki wa vituo vya soka katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wametakiwa kushikamana nikuhakikisha wanarejesha heshima na utawala wa soka katika Manispaa hiyo ikiwa pamoja na kuweka mikakati ya kukuza vipaji kupitia vituo hivyo.
Kauli hiyo ameitoa Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Mgore Miraji Wakati akizungumza na viongozi hao wa vituo vya soka ambapo amewataka kuepuka Mjungu nakuchonganisha wanapoenda kuhakikisha wanarejea utawala wa soka kama ilivyozoeleka.