#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, amekagua miradi mitatu ya maendeleo katika Manispaa ya Lindi yenye thamani ya Shilingi bilioni 15.7, inayohusisha ujenzi wa Soko Kuu, Stendi Kuu ya Mabasi ya Mitwero, na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa. Ziara hiyo ililenga kuhakikisha miradi hiyo muhimu kwa uchumi wa mkoa inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika na kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Katika ukaguzi huo, Mhe. Telack ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na kutoa maelekezo makali kwa wakandarasi kuongeza idadi ya wafanyakazi na kuweka taa ili kazi zifanyike mchana na usiku. Amesisitiza kuwa washauri wa miradi lazima wawepo maeneo ya ujenzi muda wote ili kusimamia ubora, huku akitoa muda wa wiki mbili kwa hatua fulani za ujenzi kukamilika ili wananchi waanze kupata manufaa yaliyokusudiwa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
