#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Mhe#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Mhe

#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Mhe. Ibrahim Shayo, ametoa wito kwa taasisi binafsi za afya zilizopo Manispaa ya Moshi, kuweka gharama rafiki za matibabu ili kuwawezesha wananchi wote kupata huduma stahiki za afya.

Mhe. Shayo ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la wagonjwa wa dharura (EMD) katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph iliyopo Manispaa ya Moshi.

Aidha, amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuendelea kuboresha miundombinu ya sekta ya afya nchini kwa kuzingatia viwango vya juu vya utoaji wa huduma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Sister Dkt. Hellen Kalyosudu, amesema ujenzi wa jengo hilo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 400, hatua inayolenga kuboresha na kuongeza ubora wa huduma za afya kwa jamii.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *