Mchambuzi wa masuala ya uchumi, Walter Nguma, amesema ukuaji wa uchumi wa taifa unategemea kwa kiasi kikubwa mzunguko wa fedha ndani ya mfumo rasmi wa kifedha, hali inayowezesha benki, watu binafsi na Serikali kupata rasilimali za kuendesha shughuli za maendeleo.
Amesema kuhifadhi fedha majumbani kunazuia mzunguko huo, jambo linalopunguza uwezo wa benki kukopesha wafanyabiashara na wawekezaji, hivyo kudhoofisha shughuli za uzalishaji na ajira.
Nguma amewashauri wafanyabiashara na watu wenye kipato kikubwa kuhifadhi fedha zao benki, ili zitumike kama mtaji wa kukopesha wengine na kuendesha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
✍Ibrahim Kilumbo
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates
