Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameitisha kikao cha dharura cha baraza la mawaziri la ulinzi mjini Paris kujadili dhamira ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kukiteka kisiwa kinachojitawala cha Greenland.

Afisa mmoja wa Ufaransa, amethibitisha kuwa mkutano huo ulikuwa umepangiwa kuanza saa mbili asubuhi kwa majira ya eneo hilo.

Katika chapisho la jana usiku kwenye mtandao wa X, Macron alisema kundi la kwanza la wanajeshi wa Ufaransa tayari linaelekea Greenland kushiriki katika zoezi la kijeshi lililoandaliwa na Denmark na Greenland.

Amesema kwa ombi la Denmark, aliamua kwamba Ufaransa itashiriki zoezi hilo la pamoja na kwamba kundi lingine litafuata baadaye.

Mataifa washirika yakiwemo Ujerumani, Norway na Sweden pia yameanza kupeleka wanajeshi wake Greenland kuonyesha mshikamano wao kwa Denmark na Greenland.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *