Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka watumiaji wa ndege nyuki maarufu kama ‘Drones’ kuzingatia sheria ya matumizi ya vifaa hivyo ili kuepuka maafa yanayoweza kusababishwa na matumizi holela.

Wito huo umetolewa Dimbani kisiwani Zanzibar na Mkaguzi wa Ndege Nyuki kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ibrahim Mohammed Abdallah wakati alipokuwa akizungumza kwenye Maonesho ya 12 ya Biashara yanayofanyika Zanzibar.

Amesisitiza kwamba wamiliki wa ‘Ndege Nyuki’ wanapaswa kuzisajili Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kabla ya kuanza matumizi na kushindwa kufanya hivyo ni uvunjaji wa sheria unaombatana na adhabu kali.

Amebainisha kwamba ‘Ndege Nyuki’ zimekuwa nyingi hapa nchini na bila ya kuwepo udhibiti wa kisheria na kikanuni zinaweza kudondokea kwenye mikono ya waovu na kusababisha uhalifu mkubwa kama wa kusafirisha dawa za kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *