Shughuli ya upigaji kura unaendelea katika vituo mbali mbali vya upigaji kura baada ya mchakato huo kuanza kuchelewa kutokana na hitilafu za kiufundi.
Katika vituo vingi vya kupigia kura, upigaji kura ulianza hadi saa nne baadaye kuliko ilivyopangwa.
“Mchakato wa upigaji kura ulicheleweshwa. Ilitakiwa kuanza saa Moja asubuhi, lakini tulianza karibu saa nne Kuna watu wengi hapa sasa, lakini wengine walikwenda kazini, kwa hivyo hatujui ni lini watarudi kupiga kura. Pia hatujui kama muda wa kupiga kura utaongezwa,” alisema Sydney Ibrahim, wakala wa NRM aliyezungumza na BBC.
“Upigaji kura unaendelea vizuri hapa katika Shule ya Greenhill. Hakuna matatizo na mchakato unaendelea vizuri. Ingawa masanduku ya kura yalichelewa kufika, kila kitu sasa kinaendelea vizuri,” Toteela Florence, mpiga kura alisema.
Bado haijulikani ni nini kilisababisha hitilafu hiyo ya kiufundi, japo baadhi ya wapiga kura wanashuku kuwa huenda umesababishwa na kuzimwa kwa mtandao wa intaneti nchini.
Wakati Tume ya Mawasiliano ya Uganda ilipotangaza kuzima kwa mtandao siku ya Jumanne, iliwahakikishia Waganda kwamba huduma muhimu na baadhi ya kazi muhimu za serikali hazitaathirika kutokan na hatua hiyo.
Kufikia sasa, haijulikani ikiwa saa za kupiga kura zitaongezwa.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Byabakama Simon hapo awali alisema sheria inaruhusu tume kuongeza muda wa kupiga kura katika mazingira kama haya.
#starTvUpdate
#chanzobbcswahili