SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetoa shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kuzalisha hewa tiba (oxygen) katika Hospitali ya Wilaya ya Mji Mafinga, iliyopo Halmashauri ya Mji Mafinga kama sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa Serikali wa kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya mfumo wa hewa pamoja na vile vinavyotokana na ajali za barabarani, kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya hewa tiba kwa wakati na kwa uhakika.

Mahitaji ya hewa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Mji Mafinga yameendelea kuongezeka kutokana na idadi kubwa ya wahanga wa ajali za barabarani wanaopata matibabu katika hospitali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *