Familia nchini Sudan zinasukumwa ukingoni huku “migogoro ya kikatili” na njaa vikiendelea. Mpango wa Chakula Duniani (WFP) pia umetahadharisha kuwa oparesheni zake za kibinadamu za kunusuru maisha ya wananchi wa Sudan zinasusua kufuatia uhaba mkubwa wa fedha.

Wakati Sudan mwezi huu ikiadhimisha kutimia zaidi ya siku 1,000 za vita vya ndani nchini humo  Shirika la WFP limeeleza  katika taarifa yake kuwa, “tatizo kubwa zaidi la njaa duniani na watu kuyahama makazi yao havionyeshi dalili za kupungua. Mpango wa Chakula Duniani umeeleza haya huku ukifanya kila linalowezekana kuendeleza operesheni zake dharura za kibinadamu.

Tangu kuzukavita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan mwezi Aprili 2023, Shirika la WFP limesema kuwa limeweza  kuwafikia zaidi ya Wasudani  milioni 10 wakiwemo wanawake, wanaume na watoto walio katika mazingira magumu zaidi wanaohitaji msaada wa dharura wa chakula, pesa taslimu na lishe.

Mpango wa Chakula Duniani (WFP) unaendelea kutoa misaada ya kuokoa maisha kwa wastani wa watu milioni nne kila mwezi, ikiwa ni pamoja na katika maeneo ambayo ni magumu kufikiwa katika mikoa ya Darfur na Kordofan, pamoja na majimbo ya Khartoum na Al Jazira.

Ross Smith Mkurugenzi wa WFP anayehusika na maandaliza na huduma za dharura wa WFP amesema: Shirika hilo limelazimika kupunguza mgao wa misaada hadi kiwango cha chini kabisa ili kuwafikia wahitaji mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *