#HABARI: Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza kutekeleza mradi mpya wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 125, unaolenga kumaliza kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma hiyo katika mitaa ya Kanada na Bonyokwa. Mradi huu unakuja kama ukombozi kwa wakazi wa Kata ya Bonyokwa, Wilaya ya Ilala, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kupata maji safi na salama kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku.
Utekelezaji wa mradi huu ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi wote kwa ufanisi na kwa gharama nafuu. Kukamilika kwa miundombinu hiyo siyo tu kutaimarisha hali ya upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo hayo ya Jiji la Dar es Salaam, bali pia kutaongeza tija katika shughuli za kiuchumi kwa kupunguza muda na gharama ambazo wananchi walikuwa wakitumia kutafuta maji mbali na makazi yao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.