#HABARI: Serikali ya Tanzania, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imeweka historia kwa kusaini mikataba 30 yenye thamani ya shilingi trilioni 1.2 kwa ajili ya mradi mkubwa wa kusambaza umeme katika vitongoji 9,009 kwenye mikoa 25 ya Tanzania Bara. Hatua hii inaashiria kuanza kwa safari ya kuwafikia wateja wa awali 290,300, huku Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha vitongoji vyote nchini vinapata nishati hiyo ifikapo mwaka 2030.

Kati ya mikataba hiyo, kampuni 21 za wazawa zimepewa kipaumbele huku tisa zikiwa za kampuni za nje zilizosajiliwa nchini, jambo linalolenga kukuza uchumi wa ndani. Mafanikio hayo yanakuja baada ya Serikali kukamilisha azma ya kufikisha umeme katika vijiji vyote 12,318 nchini kote hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2025.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy, amebainisha kuwa mradi huu wa sasa ndio mkubwa zaidi kuwahi kutekelezwa, ukihusisha ujenzi wa miundombinu mipana ikiwemo kilomita 13,180 za njia za msongo wa kati na ufungaji wa mashineumba 9,009. Takwimu zinaonyesha maendeleo makubwa tangu mwaka 2021, ambapo idadi ya vitongoji vyenye umeme imeongezeka kutoka 28,258 hadi kufikia zaidi ya 41,000, jambo linaloonyesha kasi ya Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi wa vijijini.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *