#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva, Januari 18, 2026, amefanya ukaguzi wa mradi wa uchimbaji wa kisima kirefu katika eneo la chanzo cha maji Sinde, Manispaa ya Lindi.

Mradi ambao unatekelezwa na wataalamu wa ndani kwa uwezeshaji wa Ofisi ya Meneja wa RUWASA Wilaya ya Lindi, kwa kushirikiana na Chombo cha Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii cha Kuchele (CBWSO).

Kisima hicho, ambacho utekelezaji wake umekamilika, kina ukubwa wa inchi 8 na kimegharimu shilingi milioni 39.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mhandisi William Swila ameeleza kuwa kisima hicho kina urefu wa mita 175 na kinatarajiwa kutoa maji lita 60,000 kwa saa moja, huku kikitarajiwa kuhudumia wananchi wasiopungua 25,000.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *