Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kwamba uchokozi wowote mpya wa kijeshi dhidi ya Iran utakabiliwa na jibu kali na la uhakika.

Araghchi amesisitiza kwamba Marekani lazima ibadilishe mwenendo wake ina iamiliane na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa msingi wa heshima ya pande zote na maslahi ya pamoja.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran ameandika makala katika jarida la Wall Street Journal na kueleza wazi kwamba, hatua za uadui zilizochukuliwa na Marekani dhidi ya Tehran zimeshindwa na kugonga mwamba.

Seyyed Abbas Araqchi, ameelezea katika makala yake hiyo kwamba maandamano ya amani yaliyofanyika nchini Iran yaligeuka kuwa vitendo vya vurugu baada ya siku chache, kufuatia kuhusika kwa mamluki wa kigaidi wa ndani na nje, na kwamba kukatwa kwa mtandao wa Intaneti ilikuwa hatua muhimu ya kudhibiti hali hii.

Katika kujadili uingiliaji wa Rais wa Marekani Donald Trump katika masuala ya ndani ya Iran, Waziri Aaraghchi ameandika? vitisho vya Trump dhidi ya Tehran, vinavyolenga kuiingiza Marekani katika vita vipya vinavyohudumia maslahi ya utawala haramu wa Israel, vimesababisha viwango vya juu vya umwagaji damu, na kwamba, ashirio la Mike Pompeo Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Marekani kuhusu ushawishi wa Shirika la Kijasusi la Israel MOSSAD ni mfano wazi wa mwenendo huu.

Aidha katika chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii wa X, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema Ulaya sasa inasumbuliwa na matokeo ya usaliti wake wa zamani kwa Iran na inakabiliwa na unyanyasaji kama huo kutoka kwa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *