#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linafanya uchunguzi wa kifo cha Gidion Mbwambo (34), kilichotokea Januari 27, 2026 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Kisanga, Mtaa wa Nguzo, Kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, tukio hilo lilibainika baada ya kuonekana kwa michirizi ya damu na maji yaliyokuwa yakitoka nnje ya Chumba Namba 106, ambacho marehemu alikuwemo.

Baada ya mlango wa chumba hicho uliokuwa umefungwa kwa ndani, kuvunjwa, marehemu alikutwa ndani akiwa amefariki dunia, huku vifaa vyenye ncha kali vikikutwa eneo la tukio, jambo lililofanya polisi kuanza uchunguzi wa kina kubaini mazingira halisi ya kifo hicho.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi unaendelea, na hatua za kisheria zitachukuliwa mara baada ya uchunguzi kukamilika.


‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *