#HABARI: Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa ataongeza ushuru wa bidhaa zinazoingizwa kutoka Korea Kusini hadi kufikia asilimia 25.
Hatua hiyo imekuja baada ya kumshutumu Rais wa taifa hilo Bwana Seoul kwa kutotekeleza ipasavyo makubaliano ya biashara yaliyofikiwa mwaka jana.
Kupitia ujumbe aliouandika kwenye mitandao ya kijamii, Trump alisema ataongeza ushuru huo kutoka asilimia 15 kwa bidhaa mbalimbali zikiwemo magari, mbao, dawa, na “ushuru mwingine wote wa kulipizana.”
Trump amesema kuwa wabunge wa Korea Kusini wamekuwa wakichelewa kuidhinisha makubaliano hayo ilhali Marekani imechukua hatua haraka kupunguza ushuru wake kulingana na makubaliano yaliyofikiwa.
Kwa upande wa Korea Kusini imesema haijapewa taarifa rasmi kuhusu uamuzi wa kuongeza ushuru kwa baadhi ya bidhaa zake, na imeomba mazungumzo ya haraka na serikali ya Marekani juu ya suala hilo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania