‎#HABARI: Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Mhe. Jacquline Mzindakaya, amehoji Serikali kuhusu hatma ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Rukwa unaotekelezwa kwa gharama ya takribani shilingi bilioni 60, akitaka kujua ni lini ujenzi huo utakamilika na kuanza kutumika.

‎Akijibu swali hilo Bungeni, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa uwanja huo, na kwamba ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo majaribio ya awali ya matumizi ya uwanja huo yataanza kufanyika.

‎Amesema kukamilika kwa mradi huo kutarahisisha usafiri wa anga katika Mkoa wa Rukwa na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii, hususani sekta za biashara na utalii.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *