#HABARI: Serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso imevifuta vyama vyote vya siasa na kufuta mfumo wa kisheria uliokuwa unasimamia uendeshaji wake, kwa mujibu wa amri iliyoidhinishwa na Baraza la Mawaziri la Taifa hilo la Afrika Magharibi siku ya Alhamisi.
Uamuzi huo uliyotolewa na utawala huo wa kijeshi chini ya Rais Ibrahim Traore, aliyeingia madaraka kupitia mapinduzi ya Septemba 2022, ni hatua ya hivi karibuni ya kuimarisha udhibiti wa mamlaka baada ya kusimamishwa kwa shughuli za kisiasa kufuatia mapinduzi hayo.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burkina Faso, Emile Zerbo, alidai kuwa mfumo wa vyama vingi ulikuwa unatumika vibaya na kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
Kabla ya mapinduzi, Burkina Faso ilikuwa na zaidi ya vyama vya siasa 100 vilivyosajiliwa, huku 15 kati ya hivyo vikiwa na uwakilishi katika bunge baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Alisema tathmini ya Serikali imebaini kuwa kuongezeka kwa idadi ya vyama vya siasa kulichochea migawanyiko na kudhoofisha mshikamano wa kijamii.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.