#HABARI: Wananchi Mkoani Geita watakiwa kuchangamkia fursa ya umeme kwenye Vitongoji vyao ambapo Wakala ya Nishati Vijijini (REA) inatarajia kusambaza umeme kwenye vitongoji 528 vitakavyo fikia jumla ya kaya 17,014 Mkoani humo.

Hayo yamesemwa leo tarehe Januari 30, 2026 mkoani Geita na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martine Shigela wakati wa kumtambulisha mkandarasi alieshinda zabuni hiyo, kampuni ya Central Electricals International Ltd itakayotekeleza Mradi huu wa kusambaza umeme kwenye vitongoji 528 vya mkoa wa Geita kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mhe. Shigela amesema ni wakati sahihi kwa Wananchi wa Mkoa huo kuchangamkia fursa hiyo na umeme usiwe tu kwa ajili ya kuchaji simu, kupiga simu na kuchati bali ikawe ni chachu ya kuongeza uzalishaji kwenye maeneo yao na itawapunguzia gharama walizokuwa wakiingi hapo awali.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *