#HABARI: Rais wa Baraza la Usimamizi wa Mkataba wa Lusaka na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, amewaagiza watendaji wa Sekretarieti ya mkataba huo (LATF) kuhakikisha idadi ya nchi wanachama inaongezeka wakati wa kipindi cha uongozi wake.
Hatua hiyo inalenga kuongeza nguvu na ushirikiano wa kikanda katika mapambano dhidi ya ujangili pamoja na biashara haramu ya nyara za serikali na rasilimali za misitu zinazovuka mipaka.
Dkt. Kijaji ametoa maelekezo hayo jijini Arusha alipokutana na watendaji hao kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja wa utekelezaji wa majukumu ya baraza hilo.
Amesisitiza kuwa atahakikisha anadumisha dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ni mhifadhi namba moja, katika kulinda urithi wa maliasili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa LATF, Bw. Edward Phiri, amepongeza ushirikiano mkubwa unaotolewa na serikali ya Tanzania katika kufanikisha majukumu ya baraza hilo tangu nchi hiyo ijiunge rasmi mwaka 1999.
Mkataba wa Lusaka ambao ulianzishwa mwaka 1994, kwa sasa una jumla ya nchi wanachama sita ambazo ni Tanzania, Kenya, Zambia, Congo Brazzaville, Lesotho, na Liberia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.