HABARI: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewatahadharisha wafanyabiashara dhidi ya tabia ya kupandisha bei za vyakula wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia vitendo hivyo.

Rais Dkt. Mwinyi amesema hakuna sababu ya msingi inayohalalisha kupanda kwa bei za bidhaa za chakula katika kipindi hicho, akieleza kuwa hali ya upatikanaji wa vyakula ipo vizuri na Serikali imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha mahitaji ya wananchi yanapatikana kwa bei nafuu.

Ameonya kuwa wafanyabiashara watakaobainika kupandisha bei kiholela watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi, huku akizitaka taasisi husika kuimarisha ufuatiliaji wa masoko ili kuwalinda wananchi, hususani wenye kipato cha chini.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *