#HABARI: Serikali, kupitia Wizara ya Nishati, imeahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa sekta ya mafuta ili kuhakikisha nchi inakuwa na nishati ya kutosha, salama, na inayouzwa kwa bei shindani.

Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Felchesmi Mramba, wakati alipokutana na wawekezaji wa kampuni za mafuta jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Mhandisi Mramba amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kutoa uhakika wa upatikanaji wa mafuta ya petroli na dizeli nchini.

Aidha, aliwashukuru wadau hao kwa ushirikiano wao mkubwa uliosaidia kudumisha utulivu wa nishati hiyo muhimu, hususan katika vipindi vya changamoto kama nyakati za uchaguzi.

Kikao hicho muhimu kimehusisha viongozi waandamizi wa Wizara, akiwemo Naibu Katibu Mkuu Dkt. James Mataragio na Kamishna wa Petroli na Gesi, Bw. Godluck Shirima.

Ushiriki wa viongozi hawa na watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara unaonyesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kusimamia sekta ya nishati kwa manufaa mapana ya Taifa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *