‎#HABARI: Taharuki imetanda katika eneo la Kakong, Kaunti ya Turkana, baada ya majangili kuwaua watu sita na kujeruhi wengine wawili katika shambulio la wizi wa mifugo.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti hiyo, John Tarus, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo yaliyomhusisha pia dereva mmoja aliyekuwa akisafiri kutoka Lodwar kwenda Kitale, huku akibainisha kuwa maafisa wa usalama wamefanikiwa kurejesha zaidi ya mifugo 1,000 iliyokuwa imeibiwa.

Kufuatia shambulio hilo, wakazi wenye hasira wamemtaka Rais William Ruto na Waziri wa Usalama wa Ndani kuingilia kati mara moja kukomesha vitendo vya ujangili vinavyowatesa.

Wananchi hao wametoa onyo kali kuwa, iwapo Serikali itashindwa kuimarisha usalama, watalazimika kujihami kwa bunduki ili kulinda maisha na mali zao, huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika chumba cha maiti cha Lodwar kusubiri taratibu zaidi.

‎Powered by #MCHEZOSUPA


‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎#Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *