#HABARI: Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela, amewataka viongozi wanaosimamia ilani ya chama kuwashughulikia vikali watu wasio waadilifu na wezi wa mali za umma.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 49 ya CCM yaliyofanyika Wilaya ya Mbeya na Mbeya Mjini, Mwaselela amesisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kujenga imani kwa wananchi na kuondoa chuki dhidi ya Serikali yao.
Maagizo hayo yanalenga kuhakikisha kuwa viongozi waliopewa dhamana wanakuwa mstari wa mbele kulinda rasilimali za taifa ili wananchi waendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi.
Sherehe hizo za kuzaliwa kwa chama zimetumika kama jukwaa la kuwakumbusha watendaji wajibu wao wa uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kutekeleza ahadi za chama kwa ufanisi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.