WAKATI dirisha la usajili Bongo likifungwa Januari 30, 2026, Yanga ikasitisha dili la kumuuza beki, Chadrack Boka, baada ya kocha wa kikosi hicho, Pedro Goncalves kusema bado anamuhitaji Mkongomani huyo.

Hapo awali Mwanaspoti iliandika kuwa Raja Casablanca, ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa Simba, Fadlu Davids, ilishusha ofa Jangwani ikitaka kumnunua beki huyo.

Lakini sasa mambo yamebadilika kwani beki huyo ataendelea kuitumikia Yanga baada ya biashara hiyo kushindwa kufanyika. Taarifa za ndani zililiambia Mwanaspoti kuwa Boka hataweza kuuzwa tena kwa sababu bado kocha anahitaji huduma yake, huku akisaidiana na Mohamed Hussein.

PED 01

“Yanga imefunga mjadala na beki wake Boka hataweza kuuzwa kwenda Raja ambayo ilikuwa inamtaka. Kocha Pedro amewaambia viongozi kuwa anataka kubaki na beki huyo, akisema changamoto zake uwanjani wataendelea kuziboresha.

Mmoja kati ya viongozi wa klabu hiyo aliliambia Mwanaspoti: “Boka bado ni mchezaji halali wa Yanga na mkataba wake haujaisha, hivyo ataendelea kuwepo kikosini.

“Kwa sasa ni ngumu kumuuza mchezaji yeyote ambaye ana kiwango kizuri kama mnavyojua tuko kwenye michuano mikubwa na migumu ya CAF, hivyo tunataka kuongeza nguvu, siyo kupunguza.”

PED 02

Boka ambaye alisaini mkataba wa kuichezea Yanga kwa miaka miwili, amesalia na miezi sita kumalizana na klabu hiyo, huku akiwa miongoni mwa wachezaji waliofanikiwa kupata nafasi ya kucheza tangu atue kikosini hapo.

Lakini kwa sasa amekuwa akigawana dakika na Mohamed Hussein, huku kwenye mechi nyingi kama hajaanza yeye basi ataingia mzawa huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *