Hilo linaripotiwa wakati kukiwa na mvutano wa kijeshi kati ya mataifa hayo mawili. Marekani lakini bado haijathibitisha mkutano wa wanadiplomasia hao wawili.

Mkutano huo iwapo utafanyika, utakuja baada ya wiki kadhaa ya vitisho vya Donald Trump kwamba ataivamia Jamhuri hiyo ya kiislamu iwapo itaendelea na kile alichokiita mauaji dhidi ya waandamanaji wa amani wanaoipinga serikali ya Tehran.

Mauaji hayo yanadaiwa kufanywa na vikosi maalum vya usalama nchini humo.

Tangu alipotoa kauli yake hiyo, Trump tayari amekwisha peleka meli kubwa ya kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati pamoja na makombora kadhaa akiwa na nia ya kuishambulia nchi hiyo kutoka baharini.

Marekani pia inajaribu kuilazimisha Iran kuachana na mpango wake wa nyuklia ulio na utata. Nchi hizo mbili zilikuwa na mkutano mwaka uliopita wa kuhusu mpango huo lakini ukashindwa kufikia suluhisho la masuala yaliyokuwa na utata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *