#HABARI: Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea mkoani Ruvuma, Mheshimiwa James Karayemaha, amewataka watumishi wa mhimili wa Mahakama, kutekeleza majukumu yao kwa unyenyekevu mkubwa na kuacha tabia ya kujitutumua, akisisitiza kuwa mwenendo huo ni msingi wa utoaji haki kwa jamii na chachu ya maendeleo ya taifa.

Mheshimiwa Karayemaha ametoa wito huo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika mjini Songea, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili, uadilifu na uwajibikaji katika utendaji wa kazi za Mahakama.

Ameeleza kuwa Mahakama ina jukumu kubwa la kulinda haki za wananchi na kudumisha amani na utulivu, hivyo watumishi wake wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuzingatia misingi ya haki bila upendeleo.

Maadhimisho ya Siku ya Sheria hufanyika kila mwaka ikiwa ni fursa ya kutathmini utendaji wa mhimili wa Mahakama na kuwakumbusha wadau wote umuhimu wa haki katika ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *