#HABARI:Katika kukabiliana na Wanyamapori wakali na waharibifu kwa Wananchi wanaozunguka Hifadhi na Mapori tengefu, Serikali imeendelea kubuni na kutumia teknolojia mseto ikiwemo uzio wa umeme ili kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi dhidi ya Tembo wanaoingia katika makazi na mashamba.

Hayo yamesemwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande, katika kikao cha 5 Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kisesa Mhe. Musa Godfrey Mbuga, aliyetaka kufahamu aina ya mbinu mpya zinazotumiwa ili kukabiliana na Tembo katika Vijiji vya Ng’hanga, Mwambongo, Matale, Longalonhinga, Sakata, Nyanza na Banhya.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *