#HABARI: Mbunge wa Tunduru Kaskazini Ndugu Ado Shaibu, amesema kitendo cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwaita Mh. Ahmed Shabiby Mbunge wa Gairo na Mhe. Kangi Lugola Mbunge wa Mwibara kinavunja Ibara ya 100 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kifungu cha 3 cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge ambavyo vinazuia chombo chochote cha dola kuwahoji wabunge kwa masuala ambayo yamejadiliwa Bungeni.

Mhe. Ado alimuomba Mhe. Naibu Spika Daniel Sillo, kutoa mwongozo juu ya suala hilo ili kulinda uhuru wa mawazo na majadiliano wa Wabunge, hata hivyo, Mhe.Naibu Spika alikataa hoja ya kutoa mwongozo juu ya suala hilo kwa sababu halijatokea mapema.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *