Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRL) imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya SGR ya Mtwara, Mbamba Bay na matawi yake ya Liganga na Mchuchuma, yenye jumla ya kilomita 1,000.

Kihenzile alitoa maelezo hayo kufuatia swali la Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye aliyehoji kwa nini serikali haioni haja ya kuanza upembuzi wa ujenzi wa reli ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Kusini kufuatia maandalizi ya mradi wa LNG.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *