Ujenzi wa shule mpya ya sekondari Ruhuhu mwambao mwa ziwa Nyasa, unatajwa kuwa huenda ukawa mkombozi kwa wanafunzi kufuatia adha walizokuwa wakizipata awali ikiwemo mimba zinazotokana na kubakwa wakiwa njiani wakifuata huduma ya elimu katika kata jirani.

Shule hii ya Sekondari Ruhuhu imekamilika na imezinduliwa na mkuu wa wilaya Olivanus Paul thomas ishara ya kuanza rasmi kutumika na tayari wanafunzi zaidi ya 100 wa kidato cha kwanza wamepokelewa na zaidi ya watumishi sabaa wa masomo yote muhimu.

Wazazi na wanafunzi wanasema kujengwa na kuanza rasmi kwa shule hii ya sekondari Ruhuhu kunatoa mwangaza wa kumalizika kwa changamoto katika sekta hiyo ya elimu ambayo wanafunzi walijikuta wakipata mimba kwa kubakwa njiani na wengine wakishindwa kuendelea kuokana na umbali kutoka walipo hadi kata jirani.

Joseph Kamonga mbunge wa ludewa anasema atahakikisha anapaza sauti bungeni ili kuisisitiza serikali kumalizia miundombinu michacche iliyosalia ikiwemo madarasa, madawati pamoja na barabara, huku akitoa ahadi kwa wanafunzi watakaofanya vizuri zaidi kitaaluma.

Kukamilika kwa shule hii kunatoa fursa kwa wanafunzi wa kata hii ya Ruhuhu na maeneo jirani kupata elimu ya sekondari ndani ya kata, hali itakayowapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata elimu katika kata ya jirani sambamba na kuepukana na matukio ya kubakwa na kusababishiwa mimba.

#RFAOnline
#HabariStartv
@dkhan1410

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *