Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Maafisa
wakuu wa Marekani na Iran wanatarajiwa kukutana Oman baadaye kwa mazungumzo ya
moja kwa moja huku kukiwa na mgogoro ambao umezua hofu ya kutokea kwa mzozo wa
kijeshi kati ya nchi hizo mbili.
Majadiliano
hayo yanakuja baada ya mzozo wa kijeshi wa Marekani Mashariki ya Kati kujibu
ukandamizaji wa kikatili wa Iran dhidi ya maandamano ya kitaifa ya kupinga
serikali mwezi uliopita, ambao makundi ya haki za binadamu yanasema uliwaua
maelfu ya watu.
Kutokuwa na
uhakika kuhusu eneo na upeo wa mazungumzo hayo kulitishia kuvuruga mazungumzo
hayo, ambayo ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia za wapatanishi wa kikanda ili
kupunguza mvutano.
Nchi zote
mbili bado zina misimamo yao. Matumaini ni kwamba, ikiwa zitafanikiwa,
majadiliano yanaweza kuchochea mazungumzo.
Marekani,
ambayo inaitaka Iran kusimamisha mpango wake wa nyuklia na kutupa akiba yake ya
urani iliyorutubishwa, ilisema mazungumzo hayo yanapaswa pia kuhusisha
makombora ya Iran, usaidizi wa nchi hiyo kwa makundi yenye silaha ya kikanda na
jinsi inavyowatendea raia wake.
Hata hivyo,
Iran imesema majadiliano hayo yatahusu tu mpango wake wa nyuklia, na
haijulikani wazi ikiwa tofauti hizi zimetatuliwa.
Katika wiki
za hivi karibuni, Rais Donald Trump ametishia kuishambulia Iran kwa mabomu
ikiwa haitafikia makubaliano. Marekani imetuma maelfu ya wanajeshi na kile
ambacho Trump amekielezea kama “silaha” katika eneo hilo, ikiwa ni
pamoja na meli ya kubeba ndege na meli zingine za kivita.
Iran imeapa
kujibu shambulizi kwa nguvu, ikitishia kushambulia mali za kijeshi za Marekani
katika Mashariki ya Kati na Israel.
Ujumbe wa
Iran utaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi, ambaye wiki iliyopita
alisema vikosi vya jeshi la nchi yake vilikuwa “vimelenga kufyatua
risasi”, huku Marekani ikiwakilishwa na mjumbe maalum Steve Witkoff na
mkwewe Trump, Jared Kushner.
Soma zaidi: