
Kiongozi mkuu wa Kishia wa Iraq, Ayatollah Ali Sistani, amelaani leo Jumatano “vita visivyo vya haki” dhidi ya Iran, vilivyoanzishwa tangu siku ya Jumamosi na Marekani na Israel. Ali Sistani, mwenyewe aliyezaliwa Iran, amewataka “Waislamu wote (…) kulaani” vita hivyo na “kuonyesha mshikamano na watu wa Iran,” akihimiza “nchi zote, hasa mataifa ya Kiislamu, kufanya kila juhudi ili kuimaliza mara moja vita hivyo na kufikia suluhu ya haki na amani ya suala la nyuklia la Iran.”
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ayatollah Ali al-Sistani ni mmoja wa viongozi wa kidini wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani wa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Yeye ndiye mamlaka kuu ya kidini (Marja’) kwa mamilioni ya Washia nchini Iraq na kwingineko duniani.
Nchini Iraq, roketi iliyorushwa dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi wa Iran yaua mtu mmoja
Mpiganaji wa Kikurdi wa Iran ameuawa katika shambulio la roketi dhidi ya Chama kinachotetea uhuru wa Kurdistan (PAK), kilichoko uhamishoni kaskazini mwa Iraq, chanzo cha chama hicho kilichoomba kutotajwa jina kimeliambia shirika la habari la AFP.
“Roketi hiyo ilipiga ngome ya PAK” katika eneo la Kurdistan linalojitawala kaskazini mwa Iran, ambalo lina kambi na vituo vinavyoendeshwa na makundi kadhaa ya waasi wa Kikurdi wa Iran.
Kampuni kubwa ya usafirishaji ya China yasitiisha shughuli zake katika Ghuba
Kampuni kubwa ya usafirishaji ya China Cosco, ambayo inaendesha moja ya meli kubwa zaidi za mafuta duniani, imetangaza kwamba inasitisha shughuli zake kwenda na kutoka nchi za Ghuba, ikiwa ni pamoja na Falme za Kiarabu, Bahrain, Saudi Arabia, Iraq, na Kuwait, kuanzia sasa.
“Kwa kuzingatia migogoro inayoongezeka katika Mashariki ya Kati na vikwazo vinavyotokana na safari za baharini katika Mlango-Bahari wa Hormuz,” Cosco imeamua “kusitisha, mara moja, shughuli … kwenye njia zilizoathiriwa hadi itakapotangazwa sheria mpya,” kampuni hiyo imesema katika taarifa.