Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, akizungumzia shambulio la mabomu lililofanywa na Marekani na Israel dhidi ya Hospitali ya Gandhi mjini Tehran, amesisitiza kuwa chini ya Sheria za Kimataifa za Kibinadamu, sekta ya afya haipaswi kulengwa kijeshi

“Vituo vya afya vinalindwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu”, amesema mkuu wa WHO kwenye ujumbe wake kwenye mtandao wa X..

“Shambulio lililolenga katikati mwa mwa mji mkuu wa Iran limeibua hofu kubwa. WHO inachunguza tukio hili. Jambo hili linatukumbusha kwamba jitihada zote lazima zichukuliwe ili kuzuia vituo kushambulia katika vita vinavyoendelea,” amesema.

Baada ya Marekani na Israel kushambulia kwa mabomu hospitali za Iran, Hossein Kermanpour, ofisa wa wizara ya afya, alitoa onyo la kina kwenye akaunti yake ya X.

“Kitabu cha ukiukwaji wa haki za binadamu katika vita hivi, kitandikwa kwa damu na aibu.”

“Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, ninashuhudia jambo ambalo sikuliona hata katika vita vya Iraq dhidi ya Iran. Wagonjwa wakiwa wamekanywa kwenye mikono ya wauguzi, wakiondolewa hospitalini katika barabara iliyojoaa moshi baada ya mabomu kulenga hospitali.”

Katika kipindi cha siku tano za vita vya kigaidi vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, hospitali kadhaa zimelengwa, jambo linaloashiria utambulisho wa kikatili wa tawala hizo mbili.

Mbali na kulenga Hospitali ya Gandhi jijini Tehran, mabaomu ya Marekani na Israel yamelenga eneo la karibu na Hospitali ya Abuzar mjini Ahvaz. Wagonjwa isa — pamoja na wale walioshikiliwa katika vitengo vya matibabu ya dharura (ICU) — walisafirishwa kwenda kwenye vituo vingine vya afya.

Kermanpour amesema: “Baada ya yaliyotokea kwenye Hospitali ya Abuzar, vituo vitatu vya matibabu ya dharura vya Sarab, Chabahar, na Hamedan, kujeruhiwa wafanyakazi wa wawili wa Huduma ya Dharura ya Afya na kuhujumiwa hospitali za Khatam, Motahari, na Gandhi mjini Tehran— kitabu cha ukiukwaji wa haki za binadamu katika vita hivi kitandikwa kwa damu na aibu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *