Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine ameishutumu Hungary siku ya Ijumaa kwa kuwateka nyara wafanyakazi saba wa benki ya Ukraine huko Budapest. Benki hiyo imesema kwamba wafanyakazi hao walikuwa wakisafirisha makumi ya mamilioni ya euro kutoka Austria.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Huko Budapest, mamlaka ya Hungary imewateka nyara raia saba wa Ukraine,” wafanyakazi wote wa Oschadbank inayomilikiwa na serikali ambao walikuwa wakiendesha magari mawili ya usafirishaji pesa kutoka Austria, Andriy Sybiga ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.

“Huu ni ugaidi na wizi unaofadhiliwa na serikali” unaofanywa na Hungary, waziri amelaani, akisema kwamba tayari ametuma barua rasmi akitaka “kuachiliwa mara moja” kwa wananchi wake.

Oschadbank imebai katika taarifa kwamba magari yake mawili yalikuwa yakisafirisha “euro milioni 35 na kilo 9 za dhahabu” kutoka Benki ya Raiffeisen nchini Austria siku ya Alhamisi, “kulingana na kanuni za usafiri wa kimataifa na taratibu zinazotumika za forodha za Ulaya.”

Magari hayo mawili ya usafirishaji pesa “kwa sasa yako katikati mwa Budapest,” benki ya Ukraine imesema, lakini mahali walipo wafanyakazi hao bado hakujulikani.

Serikali ya Hungary bado haijajibu chochote kuhusiana na madai hayo kutoka serikali ya UKraine.

Hungary ni mojawapo ya nchi chache wanachama wa NATO na Umoja wa Ulaya kuimarisha uhusiano wake na Moscow tangu mashambulizi yake makubwa yalipoanzishwa nchini Ukraine mwaka wa 2022. Budapest inazuia kupitishwa kwa kifurushi cha 20 cha vikwazo vya EU dhidi ya Moscow na utoaji wa mkopo wa euro bilioni 90 kwa Kyiv hadi itakapohakikisha kuanza tena kwa usafirishaji wa mafuta kupitia bomba la mafuta linalopita Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *