
Kituo cha kifikra cha Uingereza cha Chatham House kimekiri kwamba Rais wa Marekani, Donald Trump, amecheza “kamari kubwa ya kisiasa” kwa kuanzisha vita dhidi ya Iran.
Chatham House imesema kwamba Wademokrati wa Marekani wanaviita vita hivi kuwa ni “vita vya kwa ajili ya uchaguzi” na visivyo vya lazima, na kwamba Warepublican pia wamegawanyika sana kuhusu vita hivyo.
Zaidi ya hayo, Chatham House imesema wafuasi wa Trump wenye msimamo mkali (mrengo wa MAGA) na watu muhimu kama Tucker Carlson wamepinga hadharani mashambulizi ya Marekan dhidi ya Iran, wakiyaelezea kuwa “yanaibua hitilafu na ni ya kishetani,” yanayoakisi mgawanyiko mkubwa ndani ya kambi ya waungwaji mkono wa serikali.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez, ameutaja uchokozi wa kijeshi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran kuwa ni “kosa kubwa sana” na akisema kwamba sisi ndio “tutakaolipa gharama yake.”
Sanchez amesisitiza kwamba anaamini vita hivi vinapiganwa nje ya mfumo wa sheria za kimataifa, akisema: “Ni vizuri miongoni mwa nchi washirika kumuunga mkono mtu anapofanya jambo sahihi, na kumnyooshea kidole pale anapofanya vibaya.”