Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, pamoja na timu yake wametembelea  Shule ya Msingi Kiromo iliyopo Bagamoyo ili kukagua maendeleo ya mradi wa ukarabati unaolenga kuboresha mazingira ya kujifunzia unaotekelezwa na Airtel kama sehemu ya kusaidia elimu na maendeleo ya jamii.

Airtel pia imesema itatoa madawati mapya 250 ili kuwapunguzia wanafunzi kero   na kupunguza uhaba wa madawati shuleni hapo.

Afisa Elimu wa Wilaya (Taaluma) wa Wilaya ya Bagamoyo  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mwalimu Joseph Bureta, alipata fursa ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Airtel na timu yake katika Shule ya Msingi Kiromo ambapo pamoja na mambo mengine, alieleza furaha yake kuona namna ambavyo Airtel inavyoleta mchango chanya katika maisha ya wanafunzi wa Bagamoyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *