Mfuko wa Aga Khan wa Maendeleo ya Kiuchumi S.AMfuko wa Aga Khan wa Maendeleo ya Kiuchumi S.A

Mfuko wa Aga Khan wa Maendeleo ya Kiuchumi S.A. (AKFED), umetangaza kuingia makubaliano ya kuuza hisa zake zote (asilimia 100) kwa kampuni ya Taarifa Ltd inayomilikiwa na mfanyabishara maarufu nchini Tanzania, Rostam Aziz.

Ununuzi huo unaashiria mwisho wa miaka 66 kati ya AKFED na NMG tangu kuanza kwa kampuni hiyo mwaka 1959.

NMG ilianza kama gazeti dogo la Kiswahili lililoitwa Taifa Leo – lililonunuliwa ili kuunda vyombo vya habari huru na kutoa sauti kwa Waafrika wengi wakati wa ukoloni huku ikijitanua katika nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Uganda na Tanzania kwa kuanzidha magazeti ya kingereza, kiswahili, televisheni na radio.

NMG ilikuwa miongoni mwa kampuni za kwanza za vyombo vya habari barani Afrika kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Nairobi tangu mwaka 1973.

Kampuni ya Taarifa Ltd inamilikiwa na Rostam Azizi, mfanyabiashara, mjasiriamali na mwanauchumi wa Afrika Mashariki pia inajishughulisha na sekta mbalimbali kama
vyombo vya habari,
madini, mawasiliano
kilimo, mali isiyohamishika, miundombinu ya bandari, nishati, ujenzi.

Mfanyabishara huyo alikuwa mwanzilishi mwenza na mbia wa Kamapuni ya Mwananchi Communications Limited kuanzia 2000 hadi 2006, ambapo alianzisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, ambayo baadye yalininuliwa na Nation Media Group. Mfanyabishara huyo pia alinunua Kampuni ya Magazeti ya Habari Corporation iliyokuwa ikichapisha Magazeti ya Mtanzania na Rai.

#StartVUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *