
Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), imesema wanajeshi wake wa kulinda amani watasalia kwenye mji wa Akobo, kuwalinda raia, licha ya kutakiwa kuondoka na jeshi la serikali.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii ya UNMISS imekuja, baada ya wanajeshi wa serikali kutangaza kuanza operesheni dhidi ya vikosi vya upinzani, vinavyomuunga mkono aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa rais Riek Machar.
Kabla ya kuanza kwa operesheni hiyo ambayo, wawakilishi wa nchi za Marekani, Uingereza na Norway, wameomba kikao na rais Salva Kiir, kumwomba aachane na operesheni hiyo.
Tangu Ijumaa iliyopita, jeshi nchini Sudan Kusini lilitoa muda wa saa 72 kwa raia wa kawaida, mashirika yanayoshughulikia masuala ya kibinadamu na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuondoka katika mji huo, unaopakana na nchi jirani ya Ethiopia.
Siku ya Jumatatu, ndio iliyokuwa siku ya mwisho kabla ya kuanza kwa operesheni hiyo na tayari maelfu ya raia wa kawaida, wamekimbia makaazi yao, lakini walinda usalama wa Umoja wa Mataifa kupitia mwakilishi wao Anita Kiki Gbeho, wamesema hawaondoki kwa sababu operesheni hiyo inatishia usalama wa raia wa kawaida.
