Chanzo cha picha, Reuters
Rais Donald
Trump amehudhuria mkutano wa Wabunge wa Republican huko Miami na kusema kuwa “vitaisha
hivi karibuni”.
“Ndani
ya wiki moja wangetushambulia kwa 100%. Walikuwa tayari. Walikuwa na makombora mengi
zaidi ya mtu yeyote angefikiria, na wangetushambulia, lakini pia wangeshambulia
Mashariki ya Kati na Israel yote.”
“Na
kama wangekuwa na silaha za nyuklia, wangeitumia dhidi ya Israeli. Na hili
lingekuwa shambulizi kubwa. Ninajua walikuwa na maeneo yote ya makombora na
vifyatuaji vyote ambavyo tumeviharibu, karibu 80% kufikia sasa, tumeharibu sehemu
kubwa ya makombora. Wana kidogo sana waliobaki nayo.”
Trump aliendelea
kusema jeshi limefanya “kazi nzuri”.
“Na
makombora yamepunguzwa kwa kiasi kikubwa. Ndege zisizo na rubani zimedondoshwa,
na tunashambulia mahali wanapotengeneza ndege zisizo na rubani,” Trump alisema.
“Tunawajua
wote, na tunawamaliza kabisa. Pale, wanapotengeneza ndege zisizo na rubani.
Kazi kubwa inaendelea. Lakini tutakuwa na ulimwengu salama zaidi mara tu
itakapokamilika, na itakamilika hivi karibuni.”
Vita
havitaisha wiki hii, lakini ‘hivi karibuni’ – Trump
Akijibu
swali kutoka kwa mwandishi wa habari kuhusu muda ambao “operesheni”
ya kijeshi ya Marekani itachukua nchini Iran, Trump alirejelea alichosema awali,
operesheni hiyo itaisha “hivi karibuni” – lakini si wiki hii.
“Nafkiri
hivi karibuni. Kila kitu Iran iko nacho kimemalizwa, ikiwa ni pamoja na
uongozi wao,” alisema.
“Watu
wengi hata hawajasikia kuhusu kiongozi wanayemzungumzia (kuchukua nafasi ya
ayatollah),” Trump alisema.
Soma zaidi:
