.

Chanzo cha picha, AP

Umoja wa
Mataifa umesema kufukuzwa na kuhamishwa kwa lazima kwa watoto wa Ukraine hadi nchini
Urusi ni uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

Ripoti mpya
ya Tume Huru ya Uchunguzi ya Kimataifa kuhusu Ukraine inasema mamlaka ya Urusi “katika ngazi ya juu zaidi” imewafukuza “maelfu” ya watoto
kutoka maeneo iliyokalia ya Ukraine.

“Ushiriki
wa moja kwa moja” wa Vladimir Putin umekuwa “ukionekana tangu
mwanzo,” inaongeza.

Ukraine
inasema karibu watoto 20,000 wamepelekwa kinyume cha sheria nchini Urusi na
Belarusi.

Tume ya
Umoja wa Mataifa hadi sasa imebaini visa 1,205 vya watoto waliochukuliwa kutoka
maeneo ya Ukraine na Urusi mnamo mwaka 2022.

Asilimia
themanini ya watoto hawa bado hawajarudishwa, ripoti inasema, na wazazi na
walezi wengi hadi leo hawajui mahali walipo watoto hao.

Hii ni sawa
na kutoweka kwa lazima na kucheleweshwa kurejeshwa nyumbani bila sababu, ambayo
ni uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita mtawalia, kulingana na Umoja
wa Mataifa.

Idadi kubwa
ya watoto waliotajwa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa waliishi katika kile
kinachoitwa Jamhuri za Watu wa Donetsk na Luhansk – maeneo ya Ukraine ambayo
Moscow inadai kuyadhibiti kinyume cha sheria.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *